

Angie Martinez wa Power 105.1 Radio Marekani.

Rick Ross.
>>> “Watu siku zote wanakuwa na mitazao tofauti, ndio maana inaitwa mitazamo, na siku zote mitazamo haifanani na wala haimanishi kuwa mitazamo hiyo inamaanisha chochote, hata mimi mwanzoni walisema mimi sio mkali na siwezi kukaa kwenye game muda mrefu.. lakini leo!?” <<< Rick Ross.

Rapper huyo hakuishia hapo, aliendelea kusema kwanini Meek Mill atakua zaidi kimuziki baada ya haya kutokea…
>>> “Meek Mill atashine zaidi baada ya hapa, wala hatakufa kimuziki nalikataa hili kabisa kwasababu hivi ndio vitu vinavyokujenga kimuziki, kama hawakushambulii basi huwezi kukua hii inaonyesha kuwa ana kitu… hua pia namshauri Meek Mill, namwambia aendelee kutengeneza muziki na afanye kitu pale tu anapoona yupo tayari kufanya kitu hicho, na kama watu wamechukulia hii beef serious basi.” <<< Rick Ross.

Badaae Rick Ross akaulizwa kuhusu mtazamo wake wa nyimbo za Meek Mill, rapper huyo alikuwa na haya ya kusema…
>>> “Nyimbo za Meek Mill ni kali sana, dogo anajua… mpaka sasa nina nyimbo 6 mpya za Meek Mill kwenye simu yangu na zote ni hit songs, zote sita!” <<< Rick Ross.
0 comments:
Post a Comment