
Baada ya beef ya Meek Mill na Drake kumalizika Meek Mill alionekana kama anatafuta beef na Future… kama unakumbuka nilikusogezea stori moja ya Meek Mill wiki chache zilizopita ambapo alimtaka Dj wake kuacha kupiga nyimbo za Future kwenye show yake akidai zinamkera.

Drake.
Sasa habari ikufikie mtu wangu wiki moja iliyopita Meek Mill aliulizwa kama kuna kitu chochote kati yake na Future, rapper huyo alikataa na kusema kuwa hana tatizo lolote lile na Future na wala hatafuti beef na yeye… Sawa, je Future anahisi hivyo!?

Meek Mill & Future.
Future na Drake wameachia mixtape yao mpya na mpaka sasa inafanya vizuri Marekani,
watu wanaonyesha support kubwa kwa kudownload kwa wingi kupitia
mitandao… lakini kinachoweka headlines muda huu kuhusu mixtape hii ni
baadhi ya nyimbo zinazosikika ndani yake ambazo kutokana na mitazamo ya
mashabiki kwenye Twitter, inasemekana kuna wimbo wao mmoja ambao Future ameimba kwa lengo la kumshambulia Meek Mill!

Meek Mill.
Wimbo unaitwa ‘Big Rings’ na kwenye moja ya verse ya wimbo huo Future anasikika akisema; “wewe unarap kutengeneza vita, mimi narap kutengeneza biashara, wanaorap kwa kurushiana maneno, wanaimba blaah blaah”… sentensi ambayo imetafsiriwa na baadhi ya mashabiki kumanisha kuwa Future kama amemdharau fulani hivi Meek Mill kwa kusema yeye sio rapper mzuri.
Hizi ni baadhi ya Tweets za mashabiki nilizofanikiwa kuzinasa kutoka Twitter…



0 comments:
Post a Comment