2Face Idibia ametumia birthday yake kuwaomba watu wakubwa kwenye muziki D’banj aka Kokomaster na producer Don Jazzy kuyamaliza mambo yao na kufanya kazi tena.
2Face aliongea jambo hili kwenye jukwa na kusema yeye ni shabiki mkubwa wa kazi zao. Kwenye show hio walikuwepo wote wawili D’Banj na Don Jazzy
D’Banj aliimba ‘I’m Feeling Good’ wimbo uliotayarishwa na Don Jazzy Ft 2Face.
D’Banj alipanda kwenye jukwaa na kusema “mambo mazuri wanayopitia wasanii wa Marvin kama Korede Bello, Reekado Banks na Di’Ja yalitolewa jasho na yeye na Don Jazzy, wanapata umaarufu na kujulikana kwa mgongo wa Don Jazzy bila kuteseka so inabidi wajitume zaidi“.
0 comments:
Post a Comment