
Rapper Meek Mill ametoka jela baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitano kwenye jela ndogo huko Philadelphia kwa kosa la kukiuka masharti aliyopewa ya kutumikia kifungo cha nje.
Meek ataendelea kutumikia kifungo cha nje kwa masharti kwamba amalize kazi zake za kijamii alizopangiwa kufanya na kuhudhuria kwa washauri wa mambo ya hasira na nidhamu.
Meek Mill pia hataruhusiwa kusafiri nje ya Philadelphia mpaka amalize program hio ya ushauri kwahio ziara ya kufanya show za nyimbo mpya hakuna.
0 comments:
Post a Comment